15 Desemba 2025 - 12:54
Source: ABNA
Wanajeshi wa Israeli Wampiga Risasi Mhamiaji Mmoja wa Kizayuni

Vyanzo vya Kiebrania vimeripoti kuwa wanajeshi wa Israeli walimpiga risasi mhamiaji wa Kizayuni huko Ukingo wa Magharibi.

Kulingana na shirika la habari la Abna likinukuu Al Jazeera, vyanzo vya Kizayuni viliripoti kwamba wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walimpiga risasi mhamiaji kimakosa katika eneo la Kedumim kati ya Qalqilya na Nablus huko Ukingo wa Magharibi.

Redio ya Jeshi la utawala wa Kizayuni pia ilitangaza kuwa katika tukio hilo la risasi, mhamiaji wa Kizayuni mwenye matatizo ya akili alijeruhiwa vibaya.

Kabla ya hapo, gazeti la Yedioth Ahronoth lilidai kuwa wanajeshi wa Kizayuni walimfyatulia risasi Mpalestina ambaye alikuwa na nia ya kuwashambulia Wazayuni kwa kisu.

Hali ni kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni linadai kwamba kijana huyo aliyejeruhiwa alikuwa ameshika kisu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha